The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu: Unahitajika Umakini Kuigawa TANESCO

0


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kwamba unahitajika umakini mkubwa kama itaonekana ipo haja ya kuligawa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali la mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba, aliyedai TANESCO ifumuliwe ili kuwe na makampuni matatu ya usafirishaji, uzalishaji na ugawaji wa umeme.

 

“Shirika letu la umeme nchini linafanya kazi kubwa, linazalisha, linasafirisha na linagawa umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini, unapotaka kufanya jukumu la aina hii inabidi tuangalie sana usalama wa Taifa letu, inabidi tuangalie kwa makini, inaweza kutokea mahali mnahitaji umeme mwingi kwa kazi fulani lakini kampuni moja ikagoma kupeleka kwa sababu zake,” amesema Waziri Mkuu

Leave A Reply