The House of Favourite Newspapers

Waziri Nape Ateua Wajumbe wanne wa Bodi ya TCRA

0
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewateua Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), uteuzi ambao umeanza leo Machi 21, 2024 na utadumu kwa kipindi cha Miaka Mitano

Wajumbe walioteuliwa na Waziri ambaye ana Mamlaka hayo kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya Mwaka 2003 ni; Prof. Aloys Ntaturo Mvuma, Dkt. Hanifa Twaha Masawe, Dkt. Irene Charles Isaka na Mohamed Ame Makame

Uamuzi huo umefanyika siku chache tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya uteuzi wa Dkt. Jones Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo na Juma Hassan Reli kuwa Makamu Mwenyekiti

Leave A Reply