The House of Favourite Newspapers

Waziri Nape na Naibu Waziri wa Maji Wanogesha Usiku Wa Malkia Wa Nguvu Mlimani City

0
Malkia wa Nguvu, Rosemary Kacungira akipokea tuzo yake ya Malkia wa Nguvu (Tuzo ya Uongozi, Sekta Binafsi). Mmiliki wa kampuni ya Equity Aviation na chuo cha marubani cha Soma Aviation. 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye (Mb) akifuatilia kilele cha Malkia wa Nguvu Mlimani City.

Machi 24, 2024 kumefanyika Usiku wa Malkia wa Nguvu katika Ukumbi wa Mlimani City Hall Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye  na Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi walikuwa wageni.

Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC),  Dr Lucy Shule, Kwa zaidi ya miongo miwili kwenye maswala ya Ulinzi na usalama akipokea Tuzo ya Uongozi kwa upande wa utumishi wa umma.
Mkurugenzi Mtendaji wa @ccbrtofficial, Brenda Msangi  ambae amehudumu katika sekta ya afya kwa zaidi ya miaka 17 akipokeaTuzo ya Uongozi (Huduma za Jamii) Mlimani City kwenye kilele cha Tuzo ya Malkia wa Nguvu.
Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi (Mb) ni miongoni mwa Viongozi waliojitokeza Mlimani City.
Wlhelmina Kubingwa, Mkurugenzi wa Primina Investments ameshinda Tuzo ya uvumbuzi na ubunifu ya Malkia wa Nguvu 2024.

 Professor Esther Mwaikambo ameshinda tuzo katika Sekta ya afya, huyu daktari bingwa wa magonjwa ya watoto. Anaitwa the Tanzanian woman of many firsts (yaani mwanamke Mtanzania mwenye kwanza nyingi). Hapa alipokea tuzo yake usiku huu hapa Mlimani City Dar es Salaam


 

Leave A Reply