The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu TZ ‘Sapraizi’

0

Stori: Na Mwandishi Wetu
WAKATI kitendawili cha nani anakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiteguliwa leo mjini Dodoma ambapo jina la mtu huyo litatinga bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura, Gazeti la Amani lina jina la mtu huyo (kapuni kwa sasa), twende pamoja.

Kwa mujibu wa chanzo makini, tayari Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ aliyeapishwa kushika wadhifa huo, Oktoba 29, mwaka huu, ana jina mkononi la mtu huyo na leo litapelekwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge ili kumkubali au kumkataa.

MTAZAMO WA MAGUFULI
“Kwanza lazima mjue kwamba, Dk. Magufuli anafanya kazi kwa kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’. Hivyo ameamua kuchagua waziri mkuu ambaye naye ana spidi kali kama yeye mwenyewe au kama ya waziri mkuu wa serikali ya awamu ya kwanza, marehemu Edward Moringe Sokoine.

“Kwa hiyo, rais ameona ili afanye kazi vizuri na kwa spidi na ili aweze kutimiza ilani ya uchaguzi kama alivyowaahidi Watanzania wakati wa kampeni, mtu huyo atamfaa,” kilisema chanzo hicho.

SIFA ZAKE
Chanzo: “Lakini pia mtu huyo ambaye anakuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano, sifa zake kubwa mbili ni kutokuwa na makundi kama wengine. Lakini pia si mwana mtandao wowote. Hili nalo mheshimiwa rais ameliona likamvutia.”

AMEWAHI KUWA NAIBU WAZIRI
Kama vile haitoshi, chanzo chetu kiliendelea kudai kuwa, waziri mkuu huyo mtarajiwa amewahi kuwa naibu waziri katika serikali awamu ya nne.

JINA LITASHANGAZA WENGI
Chanzo kiliendelea kusema kuwa, jina la waziri mkuu huyo litakapotajwa bungeni na kusikika kwenye vyombo vya habari, Watanzania watashangaa sana kwani ni geni masikioni mwa wengi.

VIPI KUHUSU MAWAZIRI HAWA?
Tangu Rais Magufuli aingie madarakani, majina mengi yamekuwa yakitajwa kuwa, huenda rais atachagua waziri mkuu kutoka hapo.

HARRISON MWAKYEMBE (60)
Alikuwa Waziri wa Afrika Mashariki. Ni mmoja kati ya watu waliotajwa sana na vyombo vya habari sanjari na mitandao ya kijamii kwamba ataikwaa nafasi hiyo nyeti katika nchi.

Kuhusu Mwakyembe, chanzo chetu kikasema: “Yule hapana. Unajua tayari kuna mambo yalikaa vibaya alipokuwa Waziri wa Uchukuzi. Si unakumbuka mambo ya mabehewa? Yule hapana!”

WILLIAM LUKUVI (60)
Huyu naye anatajwatajwa sana. Alikuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya wMakazi wa serikali iliyopita. Chanzo chetu kinamwelezea hivi:

“Huyu ni mchapa kazi kweli! Inajulikana. Lakini wakati wa mchakato wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpata mgombea mmoja wa kinyang’anyiro cha urais, Lukuvi alikuwa kwenye kambi moja ambayo mgombea wake alikatwa. Ni vigumu yeye kuwa waziri mkuu. Unajua rais yeyote anataka waziri mkuu atakayemwamini kutoka moyoni mwake.”

JANUARY MAKAMBA (42)
Huyu alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia. Amekuwa akitajwa kushika wadhifa wa uwaziri mkuu kwa Rais Dk. Magufuli.

Chanzo kinamdadavua: “Makamba yupo vizuri sana tena amemsaidia sana Magufuli kwenye kampeni zake kati ya wale wajumbe 32 waliokuwa wakipita mikoani.
“Makamba ana uwezo mkubwa wa kujua mambo ya mbele na kuyawekea mikakati.

ana makundi. Lakini bado! Nafasi ya uwaziri mkuu inataka kidogo mtu mwenye kumudu kubeba mambo kiutu uzima. Na unajua kimaandiko, inaonekana kuna umri wa mtu kuweza kubeba mambo mazito. Ni wakati ambapo ameingia kwenye umri wa kufurika hekima. Makamba bado kijana sana. Afadhali angefika miaka 50 hivi.”

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply