The House of Favourite Newspapers

Waziri Ummy Apiga Marufuku Safari za Wakuu wa Mikoa – Video

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Ummy Mwalimu ametoa taarifa kuhusu Mpango wa Matumizi ya fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo amewapiga marufuku wakuu wa mikoa na wakurugenzi kutoka nje ya mkoa bila kibali cha Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. 

 

Waziri Ummy amesema hayo leo Jumanne, Oktoba 12, 2021 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma na kusema agizo hili ni ndani ya miezi hii 9 ya kukamilisha miradi ya fedha za mkopo kwa ajili ya kupunguza athari zilizosababishwa na uviko19 wakae kwenye maeneo yao kusimamia.

 

Amesema kwamba, wizara hiyo imepewa sh bilioni 535.6 sawa na asilimia 41.1 ya fedha zote zilizotolewa na Benki ya Dunia ikiwa ni mkopo wa wa masharti nafuu wenye thamani ya Sh trilioni 2.7.

 

Ummy amesema fedha hizo wamezielekeza katika kutekeleza vipaumbele mbali mbali, ambapo sh bilioni 304 imepelekwa kwenye elimu msingi ambayo ni elimu ya awali, msingi na sekondari. Pia kwa upande wa Afya zimepelekwa sh bilioni 226.6 katika kujenga vituo vya Zahanati na vituo vya afya vya Halmashauri, wakati sh bilioni 5 zimeelekezwa kuboresha miundombinu ya wafanyabiashara wadogo.

 

Ummy amesema sh bilioni 302.7 zimeelekezwa kujenga madarasa 12,000 shule za sekondari; “Tunatarajia kuwa na wanafunzi watakaofaulu milioni 1.22 kwa Januari 2022, wanafunzi hao wanahitaji vyumba vya madarasa 2,535, vilivyopo vinavyoachwa na kidato cha nne ni vyumba 8,535 kuna huitaji vyumba vya madarasa 12,000.

 

“Mikoa mitano itakayonufaika na mgao mkubwa wa fedha za benki ya dunia kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 12,000 ya sekondari ili kupambana na Corona ni Mwanza ambayo imepewa sh bilioni 19.7 ambayo itawawezesha kujenga madarasa 985. Mkoa wa pili ni Dar es Salaam ambapo imepewa sh bilioni 18. 860, Geita imepewa sh bilioni 14.840 na Morogoro imepewa sh bilioni 14.140.

 

“Tunajambo hili kubwa, ninawaelekeza viongozi wote wa Serikali ndani ya Tamisemi, ngazi ya mikoa, wilaya na halmashauri kuepuka safari zisizo za lazima zinazohusu kutoka nje ya mkoa wako isipokuwa kwa kibali cha viongozi wakuu wa nchi.” amesema Ummy.

 

Leave A Reply