The House of Favourite Newspapers

WAZIRI WA MAMBO YA NJE CHINA AWASILI NCHINI

KOMREDI Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na mamia ya wanachama wa CCM wakiongozwa na Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

 

 

Komredi Song Tao amefanya mazungumzo na Viongozi wa Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, ambapo ameendelea kusisitiza kuwa CPC itaendeleza ushirikiano na urafiki mzuri na CCM uliosisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Zedong miaka zaidi ya 50 iliyopita.

 

 

Naye Ndg. Bashiru ally Katibu Mkuu wa CCM akimkaribisha Ndg. Tao nchini Tanzania amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinathamini sana uhusiano kati ya CCM na CPC na Uhusiano mzuri sana uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China na kwa niaba ya CCM amemhakikishia Ndg. Song kwamba ushirikiano zaidi katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya vyama vyetu na wananchi wa mataifa yetu.

 

Komredi Song Tao yupo nchini kwa ajili ya Mkutano wa Kidunia wa vyama vya siasa utakaofanyika siku ya tarehe 17 na 18 Julai 2018, pia atashiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi wa Chuo cha Uongozi cha Chama Cha Mapinduzi kitakachojulika kwa jina la Chuo cha Uongozi Cha Mwalimu Julius Nyerere. Aidha, Komredi Song Tao atatembelea Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Stesheni ya Tazara.

Comments are closed.