The House of Favourite Newspapers

Waziri wa TAMISEMI Awataka Wakuu Wa Mikoa Na Wilaya Kusimamia Fedha Za Miradi

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kushuka chini kwa wananchi ili kusimamia fedha za miradi yote iliyotolewa na serikali.

Mchengerwa ametoa kauli hiyo Septemba 4, 2023 wakati akiwahutubia watumishi wa TAMISEMI baada ya kukabidhiwa Ofisi na Waziri wa zamani wa ofisi hiyo Angellah Kairuki mtumba jijini Dodoma.

Amesema serikali imetopa fdedha nyingi katika miradi mbalimbali kwa wananchi hivyo viongozi walio katika mikoa na Halmashauri za wilaya wanawajibu wa kuhakikisha kuwa wanasimamia ili kutimiza malengo ya Serikali.

Ndugu zangu naomba nisisitize kuwa dhamira ya serikali kwa sasa ni kuona kuwa kila fedha inayotolewa inafanya kazi kwa faida ya wananchi.

SHANGWE BUNGENI NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO AKIKARIBISHWA na SPIKA TULIA – ”USIWE NA WASIWASI”

Leave A Reply