visa

Waziri wa Zamani Iddi Simba Afariki Dunia

Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba amefariki dunia leo saa Alhamisi Februari 13, 2020 saa 5 asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Februari 13, 2020 Ahmad Simba amesema kaka yake aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tanu, amefariki wakati akipatiwa matibabu, “ni mshtuko kwetu kwa kweli, amefariki wakati akiendelea na matibabu.”

 

Amesema hadi saa 6 mchana walikuwa hawajakutana kupanga taratibu mbalimbali za msiba.

“Bado ni mapema kwa sasa familia inatarajia kukutana na tutajua baada ya hapo nini tutafanya kuhusu msiba na mazishi, bado hatujapanga chochote,” amesema Ahmad.
Toa comment