The House of Favourite Newspapers

Waziri Awataka Wafanyakazi Uchukuzi Wasifanye Kazi kwa Mazoea

0

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amewataka wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi kujenga tabia ya kujiendeleza kielimu ili kufanya kazi kwa weledi huku wakiacha kufanya kazi kwa mazoea.

 

Ameyasema hayo jana Jumatatu, Januari 11, 2021, kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi uliowakutanisha wakuu wa idara, vitengo na taasisi za umma zilizo chini ya sekta hiyo kwa kuzingatia muundo wa Mkataba wa Baraza ili kuimarisha ushiriki wa kweli wa wafanyakazi katika uendeshaji wa shughuli za wizara huku akiwataka kujendeleza ili kuendana na teknolojia inayobadilika.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni katibu wa sekta ya uchukuzi, Gabriel Migire, amesema lengo la kukutana ni kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati, ikiwemo miradi ya ujenzi wa reli ya kati, uimarishaji wa kampuni ya ndege, kujenga na kukarabati meli ya abiria na mizigo katika Ziwa Victoria na Nyasa.

 

Na Leah Marco, Mwanza
Januari 11, 2021.

 

Leave A Reply