The House of Favourite Newspapers

WCB Waanika ya Rich Mavoko BASATA!

LEBO ys WCB imesema taarifa za Rich Mavoko kwenda kujisali Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) si sawa kwani tayari alikuwa ameshasajili kupita lebo hiyo mwaka huu. Meneja kutokea WCB, Sallam SK amesema hayo alipokuwa akieleza ushirikiano uliyipo kati ya WCB na Baraza hilo kwa sasa.
“Suala la kusema hatushirikiani na BASATA hilo litakuwa si la kweli na sisi tunashirikiana nao sana kuna vitu vinatokea bahati mbaya. Lakini ukiangalia wasanii wetu wote wamesajiliwa BASATA na hamna yeyote ambaye hajawahi kujisajili. Hata juzi kati hapa ilisemekana kuwa Rich Mavoko ndio alienda BASATA akajisajili, hapana!, kashasajili kupitia WCB, actually mwezi wa saba mwaka huu,” alisema Sallam SK.
August 09, 2018 msanii Rich Mavoko alifika BASATA kwa kile alichoeleza alienda kujisajili na Baraza hilo lilithibitisha hilo pia.

Comments are closed.