The House of Favourite Newspapers

Wema Atoa ya Moyoni Kuhusu Uhusiano Wake na Whozu, Akataa Ndoa

0
Supastaa wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu akiwa na mpenzi wake wa sasa, Whozu.

 

WEMA Isaac Sepetu; ni supastaa wa filamu nchini Tanzania ambaye amekwenda kinyume kabisa na tangazo la boyfriend wake wa sasa, Whozu kuwa atafunga naye ndoa mapema mwaka 2023.

 

Wema ametoa ya moyoni kuhusu uhusiano wake na Whozu na uwezekano wa kufunga naye ndoa.

Wema ameweka wazi kwamba, kwamba hayupo tayari hata kidogo kuingia kwenye ndoa na Whozu kama ambavyo imetabiriwa na wengi kuwa hakuna ndoa hapa!

 

Wema anasema kuwa, huo ndiyo ukweli wake kwamba, hayupo tayari kabisa kuolewa na Whozu, na kuwaacha wengi wakijiuliza kama uhusiano wake na kijana huyo wa watu bado upo imara au ndiyo mwanzo wa nyufa kuanza kujitokeza.

 

“Mimi sijui, naona kidogo ndoa…ndoa yaani siko tayari kuolewa na Whozu,” anasema Wema.

Itakumbukwa kuwa, Wema Whozu walianza uhusiano wao takriban mwezi mmoja uliopita na wamekuwa wakipigwa vita mitandaoni ambapo wengi wanasema Wema anajidhalilisha kuingia kwenye uhusiano na Whozu ambaye wengi walimtaja kama mdogo si tu kiumri tu, bali pia kiumaarufu.

 

Wiki mbili zilizopita, Whozu alimpeleka Wema kisiwani Zanzibar kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo walijiachia kimahaba na kula bata aliyenona.

 

Sasa; ndani ya muda mfupi inashangaza kwa Wema kusema kwamba uhusiano wake na Whozu si wa muda mrefu na katu hautakuja kudumu, katika kile ambacho anadokeza kwamba bado atalazimika kurudi sokoni ili kumtafuta mwanaume wa ndoto zake.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

IRENE UWOYA AGOMEA SWALI VIDEO CHAFU ZILIZOSAMBAA MITANDAONI, AKIMBIA ‘INTERVIEW’..

Leave A Reply