The House of Favourite Newspapers

Rais wa Yanga Awahakikisha Mashabiki Kufuzu Makundi Shirikisho Dhidi ya Club Africain

0
Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said.

RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said, amewahakikisha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuwa, kikosi hicho kitafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo watulie, hawapaswi kuwa na hofu yoyote.

 

Novemba 2, mwaka huu, Yanga itashuka Uwanja wa Mkapa Dar, kukabiliana na Club Africain ya Tunisia, kisha Novemba 9, watarudiana nchini Tunisia ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi.

 

Yanga wameangukia michuano hiyo baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Al hilal ya Sudan.

 

Akizungumzia mikakati yao ya kufanya vizuri Kombe la Shirikisho Afrika, Hersi alisema wamejifunza mambo mengi baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa, hivyo wanapokwenda Shirikisho, wana matumaini ya kufanya vizuri.

 

“Nataka niwaambie ‘process’ (mchakato) ya mpira ni hatua, kwa hiyo msivunjike moyo Wanayanga, tunakwenda kwenye confederation (Kombe la Shirikisho), tayari tumejifunza baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo maeneo tuliyokuwa na udhaifu nayo, tumeyafanyia kazi.

 

“Nataka niwahakikishie kwa nguvu za Mwenyezi Mungu, tutavuka kwenda hatua ya makundi ya CAF Confederation Cup,” alisema.

MUSA MATEJA, Dar es Salaam

Leave A Reply