WEMA ATOKA NA GONJWA GEREZANI

BAADA ya kutupwa Mahabusu ya Segerea jijini Dar kwa wiki moja, Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu amedai kutoka na gonjwa lililosabisha alazwe hospitalini.  Wema aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum kuwa; “Gerezani si mahali pazuri.” Aliongeza kuwa, tangu atoke huko afya yake imetetereka, huku akituhumu mazingira mabaya aliyoyakuta mahabusu kuwa huenda yamemsababishia kupata  ugonjwa ambao haujafahamika.

“Kwanza mbu ni wengi, walining’ata sana,” alisema Wema ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alilazwa katika hospitali moja jijini Dar (jina kapuni) kwa ajili ya uchunguzi na tiba. “Nilipimwa malaria, UTI na vipimo vingine, lakini ugojwa haukubainika, alichonishauri daktari wangu ni kuwa ipo haja ya kupima vipimo vingine ili kujua.

“Aliniambia nikapime pia Dengue, kusema kweli bado naumwa hivyo ninaendelea na matibabu pamoja na uchunguzi zaidi,” alisema Wema almaarufu Tanzania Sweetheart. Hata hivyo, kabla ya kwenda mahabusu baada ya dhamana yake kufutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Miss Tanzania huyo alidaiwa kuwa alikuwa anaumwa.

Alipoulizwa na mwandishi wetu kuwa huenda ugonjwa unaomsumbua aliingia nao gerezani alisema; “Hapana, wakati naenda mahabusu nilikuwa nimeshapona muda mrefu, matatizo niliyapata huko. “Kwanza nikiwa mahabusu niliumwa sana na tumbo, kichwa na mwili kuishiwa nguvu, hadi siku natoka sikuwa sawa kiafya,” alisema Wema. Wema alikaa mahabusu kwa siku saba kwa kile kilichodaiwa na mahakamu kuwa ni kuruka dhamana kutokana na yeye kutofika mahakamani wakati wa kusikilizwa kwa shauri lake la kudaiwa kupiga na kusambaza picha zisizokuwa na maadili, kesi ambayo bado inaunguruma mahakamani hadi sasa.


Loading...

Toa comment