The House of Favourite Newspapers

Zitto Aanika Mfanyabiashara wa Kenya ‘Alivyotekwa’ Tanzania – Video

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe ameitaka Serikali ya Tanzania kuangalia kwa uzito suala la kutekwa kwa raia wa Kenya anayeishi Tanzania, Raphael Ongagi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 1, 2019 jijini Dar es Salaam, Zitto amesema masuala ya utekaji yamekuwa yakileta taswira mbaya kwa nchi ya Tanzania.

 

Amesema Tanzania haipaswi kuwa na taswira hiyo kwa mataifa mengine hasa nchi jirani ambazo tumekuwa tukishirikiana nazo katika mambo mengi.


“Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinahusishwa na matukio haya, naviomba viache mara moja au vitoke mbele vijisafishe,” amesema Zitto.

 

Akizungumzia mazingira ya kutekwa kwake, Zitto amesema siku aliyotekwa maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam Juni 24, 2019 Raphael alikuwa na mke wake Veronica wakitokea shuleni kwa mtoto wao kwenye kikao cha wazazi.

 

“Gari moja iliwazuia kwa mbele na kuwatolea silaha aina ya bastola na kuwachukua wote wawili kabla ya kumwachia mkewe na kuondoka na Raphael. Leo (Jumatatu) ni siku ya saba hatujamwona Raphael.

 

“Sisi marafiki wa Raphael Ongngi, kila tunapokwenda kufuatilia tunaambiwa ataachiwa tu tusiwe na wasiwasi. Kila tunayeongea naye Serikalini na kwenye vyombo anatuambia kuwa tutulie ataachiwa. Siku saba sasa zimepita, bado anashikiliwa,” amesema Zitto.

Comments are closed.