Wema kwa Hili la Mihela, wa Kukuoa….

NA OJUKU ABRAHAM | IJUMAA| ZA CHEMBE

WEMA Sepetu, kwangu ni miongoni mwa wasanii waigizaji wa kike wanaojua nini wanafanya wakiwa mbele ya kamera. Na samahani, siyo peke yake, wapo na wengine ninaowakubali kama Irene Paul. Ni wasichana f’lan ninaowaona wanafanya vizuri linapokuja suala la uhalisia wa kile wanachoigiza, ukiachana na wengi wanaoigiza hadi mtazamaji anakereka.

Hii siyo mara yangu ya kwanza kumzungumzia Wema katika safu hii na kwa maana hiyo, sitarudia kuzitaja sifa zake nyingi katika uigizaji wa fi lamu. Na siyo kwamba ninakutana naye hapa mara nyingi kwa sababu nina chuki naye, hapana, huwezi kuwa na chuki na mtu kama Wema, ambaye ni mkarimu kwa kila mtu, uongo?

Huyu binti ni role model wa watu wengi sana, wake kwa waume na katika akaunti yake ya Instagram, ana wafuasi zaidi ya milioni moja. Hao ni watu wengi mno, ina maana akitaka kuhamasisha kitu, wanaweza kutoa ushawishi kwa idadi nyingine kama hiyo na kitu kikasimama.

Kwa maana hiyo, mtu kama huyu ni rahisi kuweka mwelekeo anaoutaka, ndiyo maana akapata hata jeuri ya kuanzisha App yake na watu kibao wanaifuatilia. Juzi hapa nimeona kitu Wema ameandika katika akaunti yake ya Instagram, anawataka mashabikiwake wakubali ukweli kuwa yeye hivi sasa hana mpenzi, kwani uhusiano wa kimapenzi aliokuwa nao zamani, hivi sasa umeisha kwani kila mmoja ana maisha yake.

Lakini aliponikosha ni pale aliposema anawaomba wamuombee kwa Mungu apate mwanaume mzuri wa kuweza kumuoa, tena mwanaume huyo awe na mihela miiiingi!

Hapo kwenye mihela mingi ndipo paliponitatiza. Nimewahi kusema huko nyuma, kuwa Wema kwa kule majuu, unaweza kumfananisha na binti mmoja anaitwa Kim Kardashian, mtangazaji wa televisheni ambaye pia ni mke wa rapa mashuhuri duniani, Kanye West. Kuna watu wanamsema binti huyu wa Kinyaturu kuwa eti ‘ametoka’ na wanaume wengi.

Kwa taarifa yao ni kuwa Kim, kabla ya kuangukia mikononi mwa West, alishatoka na mastaa zaidi ya 25, achilia mbali wale ambao hawaeleweki. Huu ni umri wa Wema kutafuta mume mwenye busara wa kumuoa na siyo mwenye fedha kwa sababu hawa wenye mkwanja mbona amesha-hag nao sana tu? Kila mmoja anajua kuwa ili kutoka na supastaa Wema ni lazima uwe na waleti iliyonona, siyo kwa ajili ya kumpa, bali kwa sababu ya gharama za kum-handle

Nilidhani angetumia nafasi ile kuwaomba mashabiki wake, wamuombee kwa Bwana Mungu wake, ampate mume bora wa kumuoa ambaye ni mwenye hofu ya Mungu, busara, hekima na upendo, maana ndicho kitu cha msingi zaidi mwanamke anakihitaji kutoka kwa mwanaume anayempenda.

Mwanamke anayetafuta mwanaume mwenye hela, hawezi kumpata wa kumuoa, bali wa kumchezea tu kwa sababu wenye hela hawajui kupenda, atapenda wangapi wakati kila mrembo anamhitaji? Wanaume wengi wenye hela huoana na wapenzi wao walioanza nao kuhangaika pamoja, hawa wengine wanaojitokeza huku juu, huwa ni wa kupotezea tu wakati.

Hivyo nikupe ushauri mdogo wangu, kwanza umri wako wa kuolewa umeshafi ka, ni vyema na haki sasa ukatafuta mtu wa kutuliza naye mpira. Pili, usiwaze sana kuhusu hela, zinatafutwa na wewe unao uwezo wa kuzipata, ukazitumia na mumeo. Umekutana na wanaume wengi wenye nazo na wewe ukazitumia sana, hukuwekeza ili zikufae ndiyo  utampa wakati huu?

SIKIA HII: Harmorapa Afunguka Mapya Penzi la Wema, Adai Kulionja Penzi la Amber Lulu


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment