The House of Favourite Newspapers

WEMA MAHAKAMANI: Sina Matumaini Yoyote, Bora Masogange Alishahukumiwa – VIDEO

Malkia wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, amefika tena mahakamani leo kusikiliza kesi inayomkabili ya matumizi ya madawa ya kulevya, ambpo amesema upande wa mashtaka wameshawasilisha maelezo yao na umebaki upande wao kuweza kujitete ambapo kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka mwezi Mei.

 

Akiwa mahakamani hapo Wema amesema hana matumaini yoyote juu ya kesi yake isipokuwa anasubiri sheria ifuate mkondo wake, huku akisema ni bora Marehemu Agness Masogange alifanikiwa kumaliza kesi yake na akatozwa faini, lakini kwa upande wake anasubiri tu sheria ifanye kazi yake.

 

Mahakama imemkuta na hatia msanii Wema Sepetu na wafanyakzi wake wawili, kwa kosa la matumizi ya madawa ya kulevya, kesi kuunguruma Mei 14 na 15, 2018.

 

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, na kusema kwamba Wema na Wenzake wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

Comments are closed.