The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Yamkuta Huko

0

MALKIA wa Bongo Muvi, Wema Sepetu amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushambuliwa kwa maneno makali na baadhi ya mashabiki kufuatia moja ya post aliyoweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi, Januari 6, 2022. Muda mfupi tu, baada ya mrembo huyo kuweka tangazo la tiba lililoambatana na ushauri wa mambo kadhaa yanayopaswa kuzingatiwa na wanawake walijifungua kwa njia ya upasuaji.

Baadhi ya mashabiki waliokutana na post hiyo ya Wema wameonesha kutoridhishwa na kitendo cha mrembo huyo kuweka tangazo hilo hasa likiambata na picha ya mtoto mchanga aliyetoka kuzaliwa.

Wema ambaye aliwahi kushinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, amekuwa akiutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutangaza biashara mbalimbali kama sehemu ya kujiingizia kipato.

Leave A Reply