The House of Favourite Newspapers

Wenger: Nadhani Man United Hawatapaki Basi Leo

0
Arsene Wenger.

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hategemei kuona mwenzake Jose Mourinho wa Manchester United ‘akipaki basi’ katika mchezo wao wa leo kwenye Uwanja wa Emirates.

 

Leo 2:30 usiku, Arsenal itaikaribisha Man United katika mchezo wa Ligi Kuu England kwenye uwanja wake wa nyumbani.

 

Timu zote zinaingia uwanjani zikitoka kushinda mechi tatu mfululizo za Premier League, ambapo Man United wapo nafasi ya pili na pointi 32 huku Arsenal ikiwa nafasi ya nne na pointi 28.

Jose Mourinho

Alipoulizwa namna alivyo-jipanga endapo Mourinho atacheza kwa kujilinda, Wenger alisema: “Hap-ana, sifikirii kama watacheza kwa kupaki basi, wana timu bora, hawana haja ya kujilinda sana.

 

“Man United ni timu imara katika mchezo dhidi yetu nadhani watasha-mbulia sana na hawa-tajilinda muda mwingi. Utakuwa mchezo mzuri kati yetu.”

 

Hata hivyo, We-nger ambaye atapa-mbana na Man United bila straika wake, Alex-andre Lacazette, alisema hategemei Mesut Ozil kucheza chini ya kiwango eti kutokana na tetesi za kutakiwa na Man United.

 

“Lacazette anaumwa nyonga, hatocheza tunaweza kumtumia Olivier Giroud pia Sanchez (Alexis) anayeumwa misuli naye anaweza kuwa fiti, sitegemei Ozil kucheza chini ya kiwango sababu ya mambo yake ya usajili,” alisema Wenger.

Leave A Reply