The House of Favourite Newspapers

Wezi Wavunja Mahakama, Waiba Sukari…

0

POLISI mkoani Njombe imewakamata watu  wawili kwa tuhuma za kuvunja Mahakama ya Wilaya ya Njombe na  kuiba vitu mbalimbali ikiwemo sukari, kompyuta mpakato tatu na mashine ya Pos inayotumiwa na mahakama.

 

Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa, amesema  watu hao ni  Masood Mang’ombe na Hamis Ismael  na  mwingine ni aliyenunua vitu hivyo kutoka Mkoa wa Ruvuma.

 

Pia amesema wamefanikiwa kukamata mtandao wa watu wanaohusika na wizi wa vifaa mbalimbali kwenye magari zikiwemo taa, maturubai, ekseli na radio.

 

Kamanda  huyo ametoa wito kwa wananchi  kufanya kazi halali na kutojihusisha na wizi ili kuepuka matatizo.

Na Amiri Kilagalila, Njombe

Leave A Reply