The House of Favourite Newspapers

White House yataka kufunguliwa kwa njia ya misaada Gaza

0
John Kirby, mkurugenzi wa mawasiliano ya ulinzi ya baraza la usalama wa taifa la Marekani.

White House, imeunga mkono mwito wa misaada ya kibinadamu, na kufunguliwa njia ya kutoka Gaza, wakati Israel, ikongeza mashambulizi yake ya kijeshi kujibu tukio la mwishoni mwa wiki lililofanywa na wanamgambo wa Kipalestina.

Maafisa wa misaada wanasema mahitaji ya kibinadamu yanahitajika sana, na wachambuzi wanasema hakuna suluhisho rahisi kutokana na wasiwasi unaoongezeka.

John Kirby, mkurugenzi wa mawasiliano ya ulinzi ya baraza la usalama wa taifa la Marekani amesema wamezungumza na maafisa wa Israel, kuhusu mahitaji yanayo endelea ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Palestina, ambao ni waathirika vilevile.

Maafisa wa White House, wamesema wiki hii kwamba wanazungumza na Misri, kuhusu uwezekano wa njia ya misaada.

Kuna vituo viwili tu rasmi vya kutokea Ukanda Gaza, ambapo Israel, Jumanne ilishambulia kituo kikubwa kinachokwenda mpaka Misri.

VURUGU NZITO ZAIBUKA KARIAKOO -WAFANYABIASHARA WAKIWASHA LAIVU SAKATA la MOTO – NGUMI ZAPIGWA KWEUPE

Leave A Reply