The House of Favourite Newspapers

Whozu,Billnass Na Mbosso Wafungiwa Na Kupigwa Faini, Nyimbo Yao ‘Ameyatimba’.

0

Kufuatia tamko la kufungiwa na kulipishwa faini kwa wasanii watatu, Whozu, Mbosso na Bilnass lililotolewa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) jana, Novemba 4, 2023, wadau na mashabiki mbalimbali wameibua mjadala mkubwa mitandaoni.

Miongoni mwa walioibua mjadala huo, niĀ @carolndosi, mwanaharakati na influencer mkubwa, ambaye ni miongoni mwa walioanza kupaza sauti baada tu ya wimbo huo kutoka, akieleza kwamba haukuwa na maadili.

Akireply taarifa ya mwanafa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo katika mtandao wa Twitter, Carol aliandika: “Thank you Hamis. But no double standards PLEASE. Wengine pia WAANGALIWE.”

Wengine waliotoa mawazo yao, wameeleza kwamba BASATA imefanya jambo zuri kuufungia wimbo huo na kuwawajibisha wahusika lakini wakaeleza kwamba bado zipo nyimbo nyingi ambazo zinaendelea kupigwa kwenye vyombo vya habari, ambazo zimejaa matusi, zinachochea mmomonyoko wa maadili na kuenda kinyume na mila na tamaduni za Kitanzania.

Tamko la BASATA limeeleza kuwa Whozu amefungiwa miezi sita na kutozwa faini ya shilingi milioni 3 kwa kutoa wimbo wa Ameyatimba ambao una maudhui yanayokiuka maadili.

Wengine walioyatimba ni Mbosso na Billnass walioshirikishwa kwenye wimbo huo.

Leave A Reply