WIKI NYINGINE YA BETIKA HII HAPA

 

GAZETI lako pendwa linalotolewa bure la Betika kama kawaida wiki hii limeingia mtaani. Hii ni wiki ya 32 tangu kuanzishwa kwake.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, linatolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

 

Leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, ilitembelea Kinondoni, Temeke Mchicha, Vetenary na Kibasila jijini Dar es Salaam ambapo kama kawaida ilikutana na wasomaji wa gazeti hilo.

Michael John ambaye ni mmoja wa wasomaji hao, alisema: “Betika ni gazeti ambalo halina ubaguzi, ukiondoa kwamba haliwahusu vijana chini ya miaka 18, lakini pia kwa wanaohusika nalo limekuwa msaada mkubwa sana.

 

“Kuna ishu za kubeti, lakini pia matangazo mbalimbali ya bidhaa na vyuo ambapo inawapa fursa nzuri wazazi kama sisi kuona ni wapi naweza kupata kitu ninachokitaka. Betika linatusaidia sana.”

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

 

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Wanaohitaji kutangaza na Betika, wawasiliane kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe betika255@gmail.com. Pia muhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye Jengo la Global Group ambapo ndipo ofisi za Betika zipo.

Toa comment