The House of Favourite Newspapers

Kwa Wikiendi Tu, Spiderman Yaingiza Mabilioni Haya

0

WATU wapo bize kupiga pesa, wanawekeza kwa pesa nyingi sana lakini mwisho wa siku wanaingiza mabilioni ya dola. Huku watu wakiwa wamesubiri kwa kipindi kirefu, hatimaye muvi ya Spiderman Homecoming iliachiwa wikiendi iliyopita ambapo imefanikiwa kuingiza dola milioni 117 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 250 kwa Marekani tu lakini kwa duniani, kwa ujumla imeingiza dola 250 ambazo ni zaidi ya bilioni 500.

Kutokana na promo ambayo ilikuwa ikifanyika huku watu wakiisubiri kwa hamu kubwa, filamu hiyo ilistahili kabisa kuingiza kiasi hicho cha dola. Kwa ujumla, mpaka sasa muvi hiyo imeshika nafasi ya 29 duniani kwa kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kwa wiki ya uzinduzi huku katika listi nzima ikiongozwa na muvi ya Star Wars: The Force Awakens.

 

Na: Nyemo Chilongani, GPL

Leave A Reply