The House of Favourite Newspapers

Winga Mpya Simba Amtaja Benchikha Atakiwa kujituma kwenye Mazoezi

0
 WIGA mpya wa Simba, Ladack Chasambi

WIGA mpya wa Simba, Ladack Chasambi amesema ana kazi kubwa ya kuhakikisha anajituma mazoezini na kufanya vizuri kwa kila nafasi atakayopewa kucheza chini ya Kocha Abdelhak Benchikha ili kumshawishi  na kumuamini.

Chasambi amesaini mkataba wa miaka mitatu Simba na tayari amejiunga na kikosi hicho huko Visiwani Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo Wekundu hao wa Msimbazi wametinga hatua ya nusu fainali.

Akizungumza na Championi Jumatano, Chasambi alisema amefurahi kujiunga na klabu kubwa ya Simba anatambua yupo kwenye timu yenye ushindani mkubwa lakini atajituma kwenye uwanja wa mazoezi na mechi atakapopewa nafasi ili kumshawishi kocha Benchikha kumuamini.

Alisema katika nafasi yake kuna wachezaji wengi wenye uwezo ndani ya Simba lakini anaimani kujiunga ndani ya kikosi hicho ni sahihi kupata viri vya kujifunza kutoka kwa wakubwa wake ambao wako kwenye kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi.

“Sina hofu juu ya ushindani wa namba uliopo ndani ya Simba, kikubwa natakiwa kujituma  kwenye mazoezi na hata mechi nikipewa nafasi ya kucheza ili kuendelea kumshawishi kocha kunipa nafasi ndani ya kikosi chake cha kwanza.

“Ni ngumu kuingia kwenye timu na kupata nafasi moja kwa moja natakiwa kupambana, kujituma na kushirikiana na wachezaji wenzangu katika mechi na kufanikiwa tunafikia malengo yanayotarajiwa,” alisema Chasambi.

Akizungumzia usajili wake, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema usajili wa winga Chasambi utakuwa na manufaa makubwa kutokana na ubora na umri alionao.

“Hatutaki kumpa presha mchezaji wetu kijana, kocha Benchikha ameridhika na usajili wa dogo na tunamuacha afanye kazi yake uwanjani kuonyesha kile tunachokitarajia kutoka kwake akishirikiana na wachezaji wenzake,” alisema Ahmed.

INAUMIZA! HAMZA AFUNGWA JELA MIAKA 30 BAADA ya MKEWE KUMSINGIZIA KUMBAKA BINTI YAO – AKAA MIAKA 10..

Leave A Reply