The House of Favourite Newspapers

Kamati Ya Bunge Yaridhishwa Na Usimamizi Ujenzi Wa Shule Ya Nsalaga

0

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imefurahishwa na namna TAMISEMI walivyosimamia ujenzi na matumizi ya fedha kupitia mradi wa SEQUIP katika shule mpya ya Sekondari Nsalaga jijini Mbeya na kushauri iwe ya mfano nchini.

Akizungumza mara baada ya kukagua vyumba vya maabara na madarasa katika shule hiyo iliyoanza kujengwa mwezi Julai, 2023, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Denis Londo amesema wameridhishwa na usimamizi pamoja na matumizi ya fedha za mradi huo kwa kuwa madarasa na vifaa vingine ni vya viwango vya juu.

“Tumefurahi kuona Mwalimu huyu ambaye alisimamia vizuri ujenzi wa shule hii amepewa ukuu wa shule,jambo hili ni zuri na ni vyema TAMISEMI mkafanya hivi na kwa walimu wengine na pia wale waliofanya vibaya hamna budi kuwaleta hapa waje kujifunza na shule hii iwe ya mfano, ” amesema Mhe. Londo

Wakati huo huo, Mhe. Londo amewataka wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii,maarifa na wawe na nidhamu kwa walimu na wazazi kwa kuwa wamekuwa na bahati ya kuwa na shule nzuri.

Awali, akisoma taarifa ya ujenzi wa shule, Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Pascal Mlela amesema hadi kufikia Desemba, 2023 shule hiyo ilikuwa imekamilika kwa asilimia 98 na wanafunzi 269 kati ya 340 wamekwisharipoti na kuanza masomo yao.

HAJI MANARA na ZAIYLISSA WATANGAZA KUISIMAMISHA DUNIA – “BAADA ya UCHUMBA ni NDOA”…

Leave A Reply