The House of Favourite Newspapers

WINNIE HARLOW, WIZ KHALIFA SASA MTU NA MKE

MWANAMITINDO, raia wa Canada, Winnie Harlow na rapa Mmarekani,  Wiz Khalifa,  wameamua kuachia kila kitu nje wakiwaonyesha wote waaotaka kujua kwamba wao sasa ni mtu na mke au mtu na mme.

Hili lilijionyesha waziwazi majuzi  jijini Los Angeles, wakati wawili hao walipokuwa wakitoka wameshikana mikono baada ya mechi ya mpira wa kikapu (basketball) kati ya Lakers’ waliochapwa na Rockets na baadaye kutokea vurugu kati ya timu hizo.

Mke wa zamani wa Wiz, mwanamitindo maarufu, Amber Rose, anasemekana ametoa kibali cha wawili hao kusonga mbele.

Image result for winnie harlow and wiz khalifa

 

Si hivyo tu, mastaa hao wamekuwa wakionekana kuwa kwa karibu zaidi kila kukicha.

 

Masaa 3 Lema Kuhojiwa POLISI Kuhusu MO Atoka na Kutema cheche

Comments are closed.