The House of Favourite Newspapers

Wizara ya Fedha Yaipongeza CMSA Kutunuku Watendaji Wanaokidhi Kimataifa

0
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande,(katikati) akiwa katika hafla ya kutunuku vyeti wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji inayokidhi viwango vya kimataifa, Kushoto ni Afisa amatendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA)CPA. Nicodemus Mkama, kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya CMSA Dk. John Mduma.

NAIBU Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, ameipongeza Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) kwa kuendesha kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji inayokidhi viwango vya kimataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya utoaji vyeti kwa watendaji hao,iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu (BOT)
Chande, amesema sekta ya fedha ina wadau wengi wanaounga juhudi za serikali kutekeleza mikakati ya kisera, kisheria na kiutendaji.

Baadhi ya wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji inayokidhi viwango vya kimataifa.

 

“Utoaji wa elimu ya fedha kwa umma na kujenga uwezo wa wataalam wanaokidhi viwango vya kimataifa ni nguzo muhimu ya utekelezaji Mpango Mkuu wa Maendeleo ya sekta ya fedha,”

“Mpango huo wa 2019/20-2029/30 wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa fedha kwaajili ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu,”amesema Chande.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, akizungumza katika hafla hiyo.

 

Aidha amesema weledi na ujuzi waliopata wahitimu hao utaleta ushindani wa kimataifa katika utendaji kazi wa sekta ya masoko
na mitaji nchini.
“Ninaamini kwamba wahitimu wa kozi hii watashiriki kutoa ushauri na kuwezesha utoaji wa bidhaa nyingi hivyo kupanua wigo kwa wawekezaji katika masoko ya mitaji,”amesema.

Pia amesema CMSA kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Uwekezaji na Dhamana (CISI) ya London Uingereza, zimetoa wataalam wanaokidhi viwango vya kimataifa na kutoa matokeo chanya na thamani ya uwekezaji wa masoko ya mitaji kufikia trilioni 36.4.

Naibu Waziri wa Fedha,Hamad Hassan Chande, akintunuku mhitimu cheti cha watendaji wa juu wanaokidhi viwango vya kimataifa, anayeshuhudi ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, CPA.Nicodemus Mkama.
Mkuu wa Mipango,Ofisi ya Umoja wa Ulaya (EU),Bi Mihaela Marcu, akihutubia hafla hiyo.
Leave A Reply