The House of Favourite Newspapers

Wolper: Acha Nionekane Chizi Kwa Rich Mitindo!

0

MALKIA wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe, amesema kuwa, yupo tayari aonekane chizi, kwani amedata kinoma kwenye penzi la Rich Mitindo.

 

Wolper ameiambia IJUMAA SHOWBIZ kuwa, watu wengi wanamuona kama chizi kwenye penzi hilo, kwani amejitosa moja kwa moja huku akiwa haambiliki wala hasikii la mtu.

“Acha waniite chizi, lakini ukweli ni kwamba, sasa hivi nimenasa kwenye huba la kweli nililolitafuta siku nyingi sana na sikuwahi kulipata,” anasema Wolper ambaye huko nyuma, hakuweza kudumu kwenye penzi kama ilivyo sasa kwa Rich Mitindo

Leave A Reply