The House of Favourite Newspapers

Wolper Ajiweka Kando na Wanaume

0
Staa wa filamu Bongo Jacqueline Wolper

STORI: MAYASA MARIWATA, IJUMAA, STAR MIX

STAA wa filamu Bongo Jacqueline Wolper amesema kuwa, japo wanaume wengi wenye nazo wamekuwa wakimsumbua kumtaka kimapenzi, haoni haja ya kuwa nao kwa kuwa anaamini ni wasumbufu tu hawana mapenzi ya kweli.

Akizungumza mawili-matatu na Star Mix, Wolper alisema, kutokana na upendo wa kweli anaojitahidi kumuonyesha mwanaume anapokuwanaye kwenye uhusiano na kujikuta akiambulia maumivu, ameona bora aweke kando masuala ya mapenzi na kuwa`bize’ na kazi zake. “Sina mpenzi kwa sasa nimeona bora niweke pembeni haya mambo nidili na kazi zangu tu ndo muhimu, nikipenda hawa wanaonisumbua `now’ nitapenda na nitakuwa kimapenzi, lakini bado wote wanaonisumbua hakuna aliyefaulu kunishawishi niwe naye,” alisema Wolper

Leave A Reply