WOLPER Akoma Kutoa Penzi Kwa Masikini – VIDEO

Jacqueline Wolper.

MUIGIZAJI mwenye mashine zake za kushona nguo mjini, Jacqueline Wolper ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa kamwe hawezi kutoa penzi kwa mwanaume masikini au mshamba kwani wao ndiyo waliomuumiza na kutaja dau la shilingi milioni 10.

 

Wolper aliiambia Za Motomoto kwa sasa hivi amekuwa ‘matawi ya juu’na hana muda wa kusumbua vichwa na wanaume washamba ambao hata kwenye kutoa hela wanashindwa.

“Wanaume masikini na washamba ndiyo waolisumbua kichwa changu, mimi sasa hivi nadili na mtu ambaye anaweza kunipa milioni 10 kwenda mbele kwenye matumizi yangu yaani kiufupi sasa hivi ni matawi ya juu, “ alisema Wolper ambaye ni mmoja wa wasanii waliokuwa visiwani Zanzibar kwa ajili ya ‘projekti’ ya Swahiliflix


Loading...

Toa comment