The House of Favourite Newspapers

WOLPER AOKOKA, AFUNGUKA KILICHOMKIMBIZA BONGO!

Jacqueline Wolper

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper hivi karibuni ametangaza kuokoka na kusema kwamba kwa sasa anampenda Yesu na anamtumikia huku akieleza pia kilichomkimbiza Bongo na kuweka makazi nchini Kenya.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Wolper alisema ameamua kuokoka kwa sababu anatambua mbali na maisha ya duniani kuna maisha ya mbinguni, kwa hiyo ni vyema akaandaa maisha hayo pia na siyo kujisahau kana kwamba hataondoka duniani.

“Kiukweli kwa sasa nimeamua kuokoka na kumrudia Mungu, nina uhakika kwa kufanya kwangu hivi niko kwenye mikono salama na mambo yangu yataninyookea zaidi kuhusu uvaaji wangu siyo tatizo kwa sababu siku hizi tunaokoka kisasa,” alisema Wolper.

Akizungumzia kilichomkimbiza Bongo na kujichimbia Kenya, Wolper alisema ni masomo kwani kwa sasa anasomea masuala ya ngozi na urembo.

Stori: Boniphace Ngumije,

Comments are closed.