The House of Favourite Newspapers

Wolper Atokwa Povu la Funga Mwaka Kisa Jino la Silver

MWANADADA mwenye mvuto kwenye tasnia ya Filamu za Bongo, Jacquiline Wolper amewafungukia wanaochukua picha zake na kuzi-edit huku wakimchafua kuhusu jino lake analodai kuwa limetengenezwa kwa madini ya Silver.

Staa huyo ambaye ni maarufu pia kwa kutupia pamba za maana amedai kuwa alitumia gharama zake kupanda ndege kwenda Sauzi kuweka jino la silver huku akiwaita ‘Kunguni’ wanaomfanyia mchezo huo mchafu.

 

Ngoja niwaeleze kitu kimoja ambacho amkijui kuhusiana na hili pengo…hli pengo nimelipandia ndege kwenda south kulitoa nakuweka ma slver kwa meno yangu kwa mahaba yangu mwenyewe ya kuwa na mwanya wa pembeni 😂😂sasa we kunguni unayetokea pasipojulikana unakuja kuchukua pcha naku edt unavyojua wewe ukizani nitakasirika au nitaumia am soleeee 🙄…unapoteza muda wako me najipenda nilivyo naikitokea nimechoka nitanyanyua makalio yangu hapa nitajilipia nauli nakwenda kuweka jino niwe na jino so plz usitokwe na damu juu ya hlo pengo langu ndilo nalodangia kwa tarfa yako kma ulikua ujui😂😂😂🔫#Pengodanga💃🥂🍾
……

Alichokiandika Wolper kwenye Instagram page yake.

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M

Comments are closed.