The House of Favourite Newspapers

WOLPER – Pesa za Kuhongwa Zina Mikosi

0

MKALImwingine kutoka uwanda wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe amesema, hakuna pesa zenye mikosi kama za kuhongwa na mwanaume.

Wolper amesema pesa za dizaini hiyo huwa zina mikosi mingi na mtu huwezi kuzifanyia kitu cha maana.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Wolper amesema kuwa, zamani baadhi ya wanawake walikuwa wakifurahia pesa za kuhongwa, lakini ukweli ni kwamba hata ukitafuta mwanamke aliyefanikiwa kwa kuhongwa ni vigumu mno kumpata.

 

“Mimi mambo ya kusubiria pesa za kuhongwa, niliyafuta kabisa kwenye kichwa changu ndiyo maana nimekuwa na nguvu ya kufanya kazi zangu kwa umakini.

 

“Mimi pesa za kuhongwa sizitaki kabisa kwani zimejaa mikosi,” anasema Wolper.Staa huyo aliongeza kuwa, kazi yake ya ushonaji na kuuza vitenge kwenye duka lake lililopo Sinza-Makaburini jijini Dar, imemfanya kujulikana hadi nje ya nchi na pia anawaanda wasichana wengine wadogo waweze kujitegemea wenyewe na siyo kutegemea pesa za kuhongwa.

STORI:IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply