The House of Favourite Newspapers

Wolper: Tunaongeza Mtoto Mwingine Soon

0

Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe ameweka wazi kuwa, wanasubiri kidogo mtoto wao akue, wapange tena na mchumba wake, Rich Mitindo kuongeza tena mtoto mwingine soon maana tangu mtoto wao huyo azaliwe, amezidisha furaha na amani ndani ya nyumba yao.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Wolper anasema kuwa, hakuna raha ambayo ameipata tangu azaliwe kama kumshika mtoto wake mwenyewe na kucheza naye, jambo ambalo linampa hamasa kubwa ya kuongeza mtoto mwingine fasta.

 

“Asikwambie mtu, kulea na kushika mtoto wako ni raha sana, nawaombea sana wanawake wezangu kila mmoja apate mtoto wake maana hapa nainjoi sana tena sana na tuna mpango na Richie mtoto wetu akikua kidogo tu, tunaongeza mwingine soon maana hii ndiyo fahari yetu,” anasema Wolper ambaye anamlea mwanawe wa kwanza aitwaye Paskali au P.

Leave A Reply