The House of Favourite Newspapers

Aggness wa Mahari Milioni 500 Kuziba Pengo la Mdee

0

MSANII wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Aggness Suleiman almaarufu Aggy Baby anasema kuwa, anajipanga kunako gemu kwa ajili ya kuendeleza pale alipoishia Vanessa Mdee aliyetangaza kukaa pembeni kidogo kwenye muziki.

 

Katika mahojiano maalum na IJUMAA SHOWBIZ, Agyy Baby ambaye pia ni maarufu kwa kigezo chake cha kutaka mahari ya shilingi milioni 500 ili aoelewe, anasema hadi sasa amepata mapokeo mazuri kupitia ngoma yake ya Wanipa ambapo ndoto yake kubwa ni kuziba pengo la Vanessa.

 

“Nimejipanga vizuri, nina sauti na ninajua kuandika mashairi kama Vanessa, nipo tayari kuziba pengo lake kwenye gemu,” anasema Aggy ambaye hivi karibuni alibadili gia ya kutaka mahari ya shilingi milioni 500 na kutaka aolewe bure na msakata kabumbu wa Yanga, Fei Toto.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply