The House of Favourite Newspapers

YAJUE MAISA YA UTOTONI YA SNURA

SNURAMWANAMUZIKI wa miondoko ya mdu­ara, Snura Mushi ameifunua siri ambayo wengi hatuijui, eti kwenye makuzi yake alikuwa ni mvivu sana kiasi kwamba kila alipokuwa akitumwa na wa­zazi wake alikuwa akisingizia kuumwa.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Snura alisema haku­wahi kupenda kutumwatumwa, alikuwa ni mvivu na kila al­ipoagizwa kufanya jambo alizua ugonjwa wa tumbo ili tu asifanye kazi husika.

 

“Uvivu huu acheni tu, sasa hivi nikikumbuka najiona mjinga, nilimsumbua sana bibi yangu kwa kusingizia ugonjwa, kila nikiona sasa natumwa naibua ugonjwa ambao sikuwa nao, bibi alinionea huruma na ku­nitungia jina flani kwani niliumwa kila siku,” alisema Snura am­baye kwa sasa anajituma sana kufanya kazi.

 

Stori: Hamida Hassan

Watoto Waliowashinda WEMA na GABO Kwenye Tuzo Wafunguka “HATUKUTEGEMEA”

Comments are closed.