The House of Favourite Newspapers

Yamoto kuja na sapraizi Dar Live

0

YAMOTO-BAND-2BAADA ya kufanya poa hivi karibuni nchini Marekani, bendi inayotikisa Bongo, Yamoto inatarajiwa kuja na sapraizi kibao kwa mashabiki wao, Desemba 19, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Amani, mratibu wa shoo hiyo, Mohamed Seif ‘Mudy K’ alisema mbali na sapraizi hizo pia watamtambulisha kwa mara ya kwanza Mshindi wa Bongo Star Search (BSS 2015) Kayumba Juma siku hiyo sambamba na Yamoto kuachia ngoma mpya baada ya Cheza kwa Madoido ijulikanayo kama Imo.

“Kutakuwa na sapraizi kibao ambapo Baby J kutoka Zanzibar kwa mara ya kwanza atatambulisha wimbo mpya, familia yote ya Mkubwa na Wanawe itahamia Dar Live,” alisema Mudy K na kusisitiza kuwa kiingilio kitakuwa 10,000 tu.

Leave A Reply