The House of Favourite Newspapers

Faiza: kivazi cha mwaka huu kitawapa presha

0

Faiza AllyMREMBO Faiza Ally, ambaye amejizolea umaarufu baada ya kutinga ukumbini akiwa amevaa ‘Pampers’ siku ya kuzaliwa kwake,amefunguka kuwa kivazi kingine akachokivaa Desemba 19, Fukwe za Coco Aqua kitawapa presha watu wengi kutokana na kuwa gumzo zaidi.

Akizungumza na kona ya Bongo Movies, Faiza ambaye ni mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi alisema kuwa siku hiyo pia itakuwa siku yake ya kuzaliwa hivyo kivazi atakachokivaa hakijawahi kuvaliwa nchini.

“Pampers iliwashangaza watu lakini kwa kweli kivazi nitakachotinga safari hii hakijawahi kuvaliwa ulimwenguni kabisa.

Nitakuwa nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa na kutakuwa na kiingilio, fedha itakayopatikana nitawasaidia watoto yatima,” alisema Faiza.

Leave A Reply