Yanga Haijakata Tamaa ya Ubingwa

ZIKIWA zimesalia mechi tano kwa upande wa klabu ya Yanga ili kumaliza Ligi Kuu Bara msimu huu, uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi kuwa bado una matumaini ya kutwaa ubingwa.

 

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 61, Simba ni kinara ana pointi 64 huku.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Matumaini ya ubingwa bado yapo kwa kuwa tuna mechi 5 ambazo tukishinda zote tunafikisha alama 15 ambazo bado zinatuweka kwenye mbio za ubingwa.“Kwa hiyo hatujakata tamaa na sasa hivi timu inaendelea kujiandaa kuelekea michezo ijayo,” alisema Bumbuli.

Stori: Simon Msinje naManzi Msosa, DSJ


Toa comment