The House of Favourite Newspapers

YANGA JEURI KUANZA NA MCHEZAJI WA SIMBA

KAMATI ya hamasa na uchangiaji ya Yanga, imemuita Mwinyi Zahera na kumwambia awape mchanganuo wa kila kitu anachohitaji. Ikabidi avute pumzi atabasamu kwanza.

 

Wakamwambia; “hatutanii wewe sema unataka mzigo kiasi gani tukupe”. Zahera akawaambia nipeni kama Mil.650 kwa kuanzia, hayo mengine tutajua juu kwa juu.

 

Kwa kuonyesha jeuri kamati ikamwambia kwamba ; “sisi tutakupa Bilioni 1 umalize kila kitu.” Zahera akazidi kupagawa kama vile haamini kinachoendelea.

 

Juzi Ijumaa walimpa taslimu Mil 80 kama kishika uchumba cha usajili wa mastaa wawili mmoja wa Ivory Coast na mwingine anacheza Kenya.

 

Spoti Xtra limejiongeza likabaini kwamba huyo wa Kenya ni yule Mnyarwanda, Jacques Tusiyenge wa Gormahia ambaye hata Simba wanamuwinda. Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra linaongoza kwa mauzo kila Alhamisi na Jumapili, imezipata ni kwamba kamati hiyo imepandisha bajeti hadi kufikia Bilioni 1.

 

“Yeye alikuwa anataka Sh.Mil 650 ili kusajili wachezaji sita wapya pamoja na kulipa gharama mbalimbali kwa kipindi cha mpito.

 

“Lakini kamati imeamua kumpa Sh.Bilioni moja ili afanye kila kitu kwa utulivu na sasa tumemruhusu kusajili wachezaji nane wapya kutoka popote anapotaka,”alisema mmoja wa vigogo
kwenye kamati hiyo iliyopania kurejesha hadhi ya Yanga chini ya Mwenyekiti, Antony Mavunde na Katibu,Deo Mutta.

 

Habari zinasema kwamba Zahera amepania kuisuka Yanga, kabla ya kuanza kwa mashindano ya Afcon,ambako yeye atakuwa kwenye benchi la DR Congo. Kigogo huyo aliieleza Spoti Xtra kwamba Zahera ameelekeza Wachezaji wenye mishahara mikubwa na viwango duni wakae nao mezani ipunguzwe kuendana na hali ya
uchumi klabuni hapo.

 

Wachezaji hao ni Juma Abdul(Sh.Mil5.6), Thabaan Kamusoko(Sh. Mil 6) na Amissi Tambwe(Sh.Mil.6). Habari zinasema kwamba Zahera huenda akapunguza wachezaji wengi kwasababu mbalimbali kwavile asilimia kubwa aliowakuta hawaendani na staili yake ya uchezaji.

 

Kocha huyo anataka wachezaji wasiopungua sita wanaotoka kwenye nchi zinazozungumza Kifaransa ambazo zipo takribvani nchi 26 Afrika.

Comments are closed.