The House of Favourite Newspapers

Yanga Kukipiga Dhidi ya Namungo Aprili 23 Uwanja wa Benjamin Mkapa

0
                                                   Kikosi cha Yanga kinachoshiriki Ligi Kuu ya NBC

KLABU ya Soka ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu ya NBC  Aprili 23 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Taarifa hizo zimethibitishwa na klabu ya Yanga kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii wa Instagram.

                           Kikosi cha Klabu ya Namungo chenye maskani yake mkoani Lindi

Taarifa za awali ni kwamba Yanga ilikuwa haina mchezo mwingine kabla ya kukutana na mtani wake wa jadi klabu ya Simba.

 

Kwa mabadiliko hayo Yanga atacheza mchezo huo jumapili ya Aprili 23 na Aprili 30 atakutana na mtani wake wa jadi katika Uwanja huohuo wa Benjamin Mkapa.

Leave A Reply