The House of Favourite Newspapers

Raia Zanzibar, Afikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Kukata Viuno Hadharani

0
                                                     Raia akiwa amevishwa pingu

Maulid Hussein Abdallah, mkazi wa Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja visiwani Zanzibar, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukata viuno hadharani.

 

Kijana huyo anatuhumiwa kutenda kosa hilo katika Mji wa Kibole, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja majira ya saa 11 jioni ambapo inaelezwa kwamba akiwa amevalia mtandio, alianza kucheza kwa kukata viuno hadharani, jambo ambalo ni kosa la kisheria visiwani humo.

 

Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba mahakama kumpa
dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi.

Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar.

 

Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama iliamuru arudishwe mahabusu hadi Aprili 25, mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi.

 

Mwanzo katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja Kisiwani Zanzibar, kwa tuhuma ya kukata viuno hadharani. Kijana huyo mkazi wa Rahaleo anatuhumiwa kutenda kosa hilo huko Kibole wilaya ya Kati, Kusini Unguja saa 11 jioni, ambapo mshitakiwa akiwa amevalia mtandio alicheza kwa kukata kiuno mbele ya hadhara jambo ambalo ni kosa kisheria.

Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba mahakama kumpa dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi.

                                   Mtuhumiwa anasubiri kujibu mashtaka juu ya tukio hilo

Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar.

Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama ilimuamuriwa kwenda rumande hadi Aprili 25 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi.

 

 

Leave A Reply