The House of Favourite Newspapers

Yanga Princess Yatakata, Simba Queens Yabanwa

TIMU ya Yanga Princess Imeanza kwa kishindo Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzanite, huku Simba Queens ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ruvuma Queens.

 

Mabao ya Yanga Princess yote matatu yalifungwa na mwanadada Mwapewa Mtumwa, huku katika sare ya mabao 2-2 mabao ya Simba yalifungwa na Mwanahamisi Omary na Joele Bukuru huku mabao ya Ruvuma yakifungwa na Protasia Mbunda na Diana Lucas.

 

Aidha, matokeo ya michezo mingine ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, JKT Queens wao waliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Baobab, Mlandizi Queens walishinda mabao 4-1 dhidi ya Panama, Alliance Girls wao waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kigoma huku TSCQ Queens wakiifunga Marsh Queens mabao 2-1.

 

Comments are closed.