The House of Favourite Newspapers

Yanga SC Kutesti Mitambo kwa Lyon

0

BAADA ya kupumzika tangu walipocheza mechi yao ya dabi dhidi ya Simba wikiendi iliyopita, leo Alhamisi jeshi la Yanga linarudi kambini rasmi kuanza maandalizi yao ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

 

Wakati kikosi hicho kikirudi kambini, kocha wao Cedric Kaze raia wa Burundi, Jumapili hii atazitesti silaha zake mbele ya African Lyon kwenye mechi ya kirafi ki itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.

 

Kambi ya Yanga ipo Kigamboni, Dar, huku ikiwa na nyota wachache kutokana na wengine kutimkia kwenye timu za taifa. Meneja wa Yanga, Hafi dh Saleh, ameliambia Spoti Xtra, kuwa: “Kikosi kinaanza kambi yake kesho (leo) Alhamisi ambapo kila kitu kuhusu kambi kiko tayari.

 

“Kuhusiana na mechi hiyo ya kirafi ki dhidi ya African Lyon, kocha Kaze mwenyewe ndiyo ameitaka na anajua juu ya malengo yake ambayo ameyapanga kuhusiana na nini atakachokiona kwenye mechi hii.”

 SAID ALLY, Dar es Salaam

 

Leave A Reply