The House of Favourite Newspapers

Yanga SC Princess Wameanza Kunoga

Mchezaji wa Yanga akifanya yake.

KOCHA Mkuu wa Yanga Princess inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake inayodhaminiwa na Serengeti lite, Hamis Kinonda, amedai kuwa itamaliza katika nafasi tatu za juu.

 

Yanga Princess ilipitia kipindi kigumu baada ya kula vichapo vikali kwenye mechi tatu mfululizo, huku moja kati ya hizo akipigwa mabao 8-1 dhidi ya vinara wa ligi hiyo JKT Queens kabla ya hivi karibuni kuamka na kuanza kuvuna pointi kwenye kila mechi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kinonda alisema; “Vijana wameshaizoea ligi baada ya kupitia changamoto nyingi mwanzo wa ligi, ndiyo maana unaona tunapata matokeo kwenye mechi zetu tunazocheza hivi sasa, nafi kiri ni jambo jema sana kwetu.

Comments are closed.