The House of Favourite Newspapers

Yanga SC yamweka kando Ibrahim Ajibu

IBRAHIM Ajibu amebakiza miezi nane kwenye mkataba wake pale Yanga, lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika ameweka wazi kuwa hawafi kirii kumuongeza mkataba mchezaji huyo kwa sasa.

 

Dar es Salaam Ajibu ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu kabla ya kukumbwa na majeruhi, mpaka sasa amefunga mabao matatu na kutoa asisti nane kwenye ligi kuu pekee.

 

Nyika ameliambia Championi Jumamosi kuwa, mipango yao kwa sasa ni kuona wanafanya vizuri katika ligi kuu na kuifanyia kazi ripoti ya mwalimu Mwinyi Zahera ya kuongeza wachezaji wapya kutokana na upungufu wa nafasi zinazoonekana.

 

“Kwa sasa mipango yetu ni kuona timu inaendelea kufanya vizuri katika mechi za ligi na kuifanyia kazi ripoti ya mwalimu ya kuongeza wachezaji wapya ambapo tupo katika mazungumzo nao.

 

“Hivyo, ishu ya kuwaongezea wachezaji mikataba kwa sasa hatuifi kirii na siyo Ajibu tu ambaye amebakisha miezi nane kuna wachezaji wengine wamebakisha miezi sita hadi mitatu lakini kwa sasa tunaifanyia kazi ripoti ya mwalimu,” alisema Nyika.

Ibrahim Mressy, Dar es Salaam

CLOUDS FM waeleza Sababu za Tigo Fiesta Kufutwa Dar

Comments are closed.