The House of Favourite Newspapers

Yanga, Simba Wapangiwa Vigogo Hawa Michuano ya CAF

Wapinzani wa Simba na Yanga katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), wamepatikana leo Jumatano ambapo ratiba kamili ya michuano hiyo imepangwa nchini Cairo, Misri.
Yanga ambaye anashiriki ya Klabu Bingwa Afrika amepangwa na timu ya St. Louis ya Visiwa vya Shelisheli huku Simba ambaye anashiriki Kombe la Shirikisho akipangwa kucheza na Gendarmerie Nationale ya Djibouti.

Michuano ya Caf inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Februari mwakani huku Yanga ikitarajia kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita huku wapinzani wao Simba wakishiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho kutokana na kuibuka mabingwa katika michuano ya Kombe la FA, msimu uliopita.

Yanga Yashusha Majembe Mawili ya Kimataifa

Comments are closed.