The House of Favourite Newspapers

Baada ya babu Seya Kutoka… Mtabiri Atoa Mpya!

Babu Seya na mwanaye wakitoka gerezani Ukonga baada ya kuachiwa huru.

SIKU chache baada ya wanamuziki, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kuachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Magufuli, mtabiri maarufu, Hussein Yahaya ametoa mpya kuhusu yanayokuja kwa mastaa, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, mtabiri huyo alisema suala la Babu Seya na mwanaye kuachiwa huru lilitabiriwa na baba yake, Yahya Hussein kabla hajafariki kwamba watatoka hata kama ikipita miaka kadhaa na kweli utabiri huo umetimia.

 

“Nakumbuka wale watoto wawili wa Babu Seya walioachiwa huru awali, baba yangu aliwaita nyumbani na kuwafanyia dua ambapo aliwaambia kwamba baba na ndugu yao atatoka.

“Yaani kipindi hicho baba yangu alikuwa hajaanza kuugua wala hakuna aliyekuwa akijua kwamba Rais Magufuli atakuwa rais, lakini utabiri wake huo umeshaonekana tayari kwani utabiri hudumu hata miaka 10 na unatimia,” alisema mtabiri.

Shehe Yahaya.

Aliendelea kusema katika ulimwengu wa mastaa bado yataendelea kutokea matukio ya kushangaza na ambayo hayakutarajiwa kama lilivyotokea kwa Babu Seya na Papii Kocha kwa kuwa mwaka huu kinyota ni wa wasanii na unamalizika Machi mwakani.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu Elizabeth Michael ‘Lulu’ kama kuna chochote kinaweza kutokea, alisema lolote linaweza kutokea kwa kuwa naye yupo kwenye tasnia ya sanaa na bado misamaha mingine itaendelea kutoka.

 

“Utabiri wangu haumlengi mtu mmojammoja bali ni makundi ya watu na mwanzoni mwa mwaka huu nilitabiri kwamba huu ni mwaka wa wasanii kupata mambo ya kushangaza, hivyo na Lulu kwa kuwa yupo kwenye sanaa lolote kuhusu kuachiwa huru linaweza kutokea,” alisema mtabiri.

STORI: Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko.

LIVE: Kinachoendelea Dodoma, Kwenye Ufunguzi wa Nyumba za Makazi, IYUMBU

Comments are closed.