The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tulieni, Mtatuelewa Tu

0

KOCHA wa viungo wa Yanga raia wa Afrika Kusini ambaye amekabidhiwa kikosi hicho kukiongoza mazoezini tangu Jumatatu ya wiki hii, Riedoh Berdien, amesema kwa moto unaoendelea mazoezini, anaamini mara baada ya usajili kukamilika na majembe yao yote mapya kutua, basi wapinzani wao wataelewa tu.

 

Kuanzia jana Jumamosi, Yanga ilitangaza kushusha vifaa vipya kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21 ambavyo tayari wameshavipa mikataba.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Berdien alisema kikosi hicho hakitaki kurudia makosa ambayo yalifanyika msimu uliopita ndiyo maana wanafanya usajili unaolenga kuifanya timu hiyo kupambania makombe.

“Tumekuwa na wiki moja bora ya maandalizi ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa 2020/21, vijana ambao tayari wameripoti kambini mpaka sasa wamekuwa na mwamko mkubwa wa kujituma kuonyesha uwezo walionao.

 

“Ni mapema sana kuongelea kuhusu viwango vya mchezaji mmojammoja kwa sasa kwa sababu bado hatujapata mchezo wowote wa kirafi ki, lakini napenda kuupongeza uongozi kwani umefanya usajili bora sana na nina imani yangu kwamba baada ya usajili kukamilika na wachezaji wote kutua tutakuwa moto wa kuotea mbali,” alisema Berdien.

Wakati huohuo, uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa taarifa ya kumfuta kazi Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa klabu hiyo, Robert Kabeya.Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, jana ilisomeka hivi:

 

“Uongozi wa Klabu ya Yanga, unawataarifu wanachama, wapenzi na umma kwa jumla kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, ndugu Robert Kabeya siyo mfanyakazi tena wa Klabu ya Yanga.

 

“Hivyo ndugu Kabeya hatakiwi kufanya jambo lolote kwa niaba ya Klabu ya Yanga na kwamba klabu haitahusika na jambo lolote litakalofanywa na mtajwa hapo juu kwa niaba ya klabu kuanzia sasa.

STORI: JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply