The House of Favourite Newspapers

Yanga Wafunguka Hatima ya Lwandamina

0
Kocha George Lwandamina.

BAADA ya kuzagaa kwa taarifa za Klabu ya Yanga kupanga kuachana na kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ameibuka na kuweka wazi hatima ya kocha huyo ndani ya kikosi hicho.

Taarifa za mwanzo ambazo zilikuwa zinasambaa zilidai kuwa Yanga wamempa mechi tano Lwandamina kama kipimo kabla ya kuachana naye kutokana na matokeo mabaya ambayo wamekuwa wakiyapata kwenye mechi zao za hivi karibuni.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Sanga amesema kuwa uongozi wao hauna nia yoyote ya kumfungashia virago Lwandamina raia wa Zambia kama baadhi ya watu ambavyo wamekuwa wakizusha juu yao kutaka kumtimua kocha huyo.

“Wala siyo kweli, kama ingekuwa kweli basi ningekwambia, lakini pia labda watu waseme mitaani, unajua watu wanasema kwa kuwa Simba wao walimpa kocha wao mechi tano, wanataka kuonyesha Yanga nao wamefanya hivi.

“Kwa mfano hiyo pafomansi unaipima vipi kwa mazingira yaliyopo kusema kweli, lakini hatujaamua wala kikao cha jana (juzi) hatujaongelea jambo hilo na wala hakijahusisha hata kidogo masuala hayo,” alisema Sanga.

 Wilbert Molandi na Said Ally.

MANJI Amshitua Okwi, Atia Neno Kuhusu Bosi Wake Huyo

Leave A Reply